Kamati ya elimu na maandalizi zinajiandaa kufanya kongamano la kimataifa awamu ya pili kuhusu udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Uongozi wa chuo kikuu cha Al-Ameed umekutana na wajumbe wa kamati ya elimu na maandalizi ya kongamano la kimataifa la chuo cha Al-Ameed awamu ya pili kuhusu elimu ya udaktari, na kujadili mambo ya kielimu na kiidara yanayo husu kongamano hilo, linalotarajiwa kufanywa tarehe 17 – 18 Novemba.

Kikao hicho kimeongozwa na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na kuhudhuriwa na wasaidizi wa rais wa chuo na wakuu wa vitivo na wasaidizi wao miongoni mwa wakuu wa vitengo.

Kwenye kikao hicho wamejadili mambo ya mwisho kuhusu kongamano la kimataifa katika chuo kikuu cha Al-Ameed awamu ya pili yanayo husu elimu ya udaktari na kujadili mamo tofauti, ikiwa ni pamoja na kukamilisha kupokea tafiti za kielimu na kuzichambua kielimu sambamba na kubaini engo zinazotakiwa kufanyiwa tafiti katika mada kuu za kielimu na kuchagua zilizo bora, na kuangalia maandalizi mengine kama vile mambo ya kiufundi, kimazingira na maandalizi ya kumbi na vifaa.

Aidha kamati ya kupokea wageni watakao shiriki kwenye kongamano hilo imepanginila majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kuratibu waongozaji wa vikao vya kielimu na kukamilisha utoaji wa mialiko kwa taasisi zitakazo shiriki, sambamba na kuwasiliana na mashirika ya madaktari kwa ajili ya kufanya maonyesho katika korido za chuo wakati wa kongamano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: