Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inaendelea kuwatahini wanafunzi wa kuhifadhi

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya inaendelea kutahini wanafunzi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu, hadi sasa imesha tahini wanafunzi (100).

Mitihani hii ni sehemu ya kupima kiwango cha wanafunzi katika kuhifadhi, na kuwaandaa vizuri kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Wasimamizi ni walimu waliobobea katika fani za Qur’ani, ambao wamekua pamoja na wanafunzi hao tangu mwanzo.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu, hufanya harakati nyingi zinazo husu Qur’ani, sambamba na semina endelevu za kuhifadhisha Qur’ani.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani na kuchangia katika kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani na uwezo wa kufanya tafiti za Qur’ani katika sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: