Inatokea hivi sasa: Kuanza kwa kongamano la kimataifa Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya asubuhi ya siku ya Alkhamisi mwezi 14 Rabiul-Awwal 1443h sawa na tarehe 21 Novemba 2021m, imeanza awamu ya pili ya kongamano la kimataifa chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takatufu) na anuani isemayo: (Historia ya Mtume katika Qur’ani tukufu na riwaya sahihi) kongamano hilo litafanyika kwa siku mbili likiwa na washiriki wa kitaifa na kimataifa.

Kongamano limefanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, limehudhuriwa na katibu mkuu na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na maraisi wa vitengo, na wawakilishi wa Ataba tukufu pamoja na kundi la wasomi na watafiti, limefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Muslimu Shabakiy iliyofuatiwa na surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).

Baada yah apo ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, uliowasilishwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Shekh Ali Mujaan, ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi uliowasilishwa na mkuu wa Daarul-A’dham -s.a.w.w- Dokta Aadil Nadhiir, halafu ukafuata ujumbe kutoka nchi washiriki za nje ya Iraq, ambazo zipo kumi nazo ni: (Misri, Sirya, Lebanon, Moroko, Aljeria, Sudani, Baharain, Iran, Malezia, Marekani), ulio wasilishwa kwa niaba yao na Dokta Ahlaam Hassan kutoka Baharain.

Katika ratiba ya kongamano kutakua na video inayo onyesha harakati za Daaru kisha kikaanza kikao vya uwasilishaji wa mada za kongamano kilicho ongozwa na Dokta Hassan Hamiid Fayaadh, ambapo mada mbili zimewasilishwa, mada ya kwanza inasema: Riwaya za historia, katika mtazamo wa Qur’ani tukufu na Habari sahihi, imewasilishwa na Dokta Mushtaqu Ghazali, ya pili inaitwa: Mwisho wa historia ya Mtume, mji wa Madina kama mfano (Maasumina na ukaribu wao na Qur’ani) imewasilishwa na Dokta Ali Shukri.

Vikao vitaendelea jioni ya leo na kuwasilishwa mada tofauti na wasomi kutoka ndani na nje ya Iraq, chini ya mada maalum za kongamano zifuatazo:

Mada ya kwanza: Historia ya Mtume mtukufu kabla ya Utume katika Qur’ani tukufu na riwaya sahihi.

Mada ya pili: Historia ya Mtume mtukufu baada ya Utume katika Qur’ani tukufu na riwaya sahihi.

Mada ya tatu: Vita za Mtume (s.a.w.w) na misafara yake katika Qur’ani tukufu na riwaya sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: