Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imefungua semina ya Qur’ani katika somo la tajwidi na usomaji sahihi

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, inafanya semina ya Qur’ani ya kanuni za tajwidi na usomaji sahihi.

Maahadi imezowea kuandaa semina tofauti za Qur’ani kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mwaka mzima, semina hizo huanza baada ya miezi miwili, mwezi wa Muharam na Safar, na baada ya kumaliza mradi wa kuwafundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu mazuwaru wa ziara ya Arubaini, uliopata mwitikio mkubwa kwa jamii na wanufaika.

Hii ni moja ya semina nyingi zinazo fanywa na Maahadi kwa ajili ya kukuza kiwango cha usomaji, kwa kufundisha hukumu za usomaji sahihi na uzingatiaji wa hukumu za tajwidi.

Wanasemina watahudhuria darasani siku mbili kwa wiki, watafundishwa na Ustadh Sayyid Dhulfiqaar Saburi.

Kumbuka kuwa semina zinazofanywa na Maahadi ni sehemu ya harakati zake muhimu, uongozi wa Maahadi unazipa kipaombele maalum kutokana na faida kubwa inayopatikana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: