Maktaba ya Ummul-Banina ya wanawake inasherehekea kuzaliwa kwa Mtume wa mwisho

Maoni katika picha
Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume wa mwisho Mhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume (s.a.w.w) ni rehema kwa walimwengu na taa kwa watembeao) na kuhudhuriwa na wanawake kutoka ndani na nje ya Maktaba.

Kiongozi wa maktaba bibi Asmaa Ra’du ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ni kawaida ya maktaba kuhuisha matukio ya kidini, ambapo huwa na aina tofauti za uhuishaji kutokana na aina ya tukio, leo tunaadhimisha kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w)”.

Akaongeza kuwa: “Kongamano lilikua na vipengele vingi, kikiwemo cha kujadili miujiza iliyotokea wakati wa kuzaliwa kwake (s.a.w.w) na njia za kusambaza mafundisho yake kwa kila rika”.

Akaendelea kusema: “Hafla hiyo imeshuhudia shindano la kaswida za mashairi ya kumsifu Mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) katika mazingira ya shangwe na furaha”.

Wahudhuriaji wameshukuru na kupongeza kazi kubwa inayofanywa ya kuadhimisha tukio hili, aidha wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari vya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) kupitia njia tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: