Kitengo cha miradi ya kihandisi kinaendelea na mradi wa ujenzi wa hospitali ya Zaaki

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na mradi wa ujenzi wa hospitali ya Zaaki katika mkoa wa Baabil, baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka mitano, hatua ya mwisho ya ujenzi huo ilikua ni kukamilika kwa umbo la jengo kuu na sehemu kidogo ya ukataji wa vyumba.

Rais wa kitengo Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa, jengo kuu linakatwa vyumba na kufungwa nyaya za umeme na fremu za madirisha na milango zinawekwa katika ghorofa zote pamoja na kuweka mfumo wa viyoyozi katika tabaka la chini”.

Akaongeza kuwa: “Jengo linalo jengwa sambamba na hilo tayali tumekamilisha hatua ya kuchimba msingi na kumwaga zege, pamoja na kupima uwezo wa msingi huo, tumeweka janvi la msingi lenye ukubwa wa (sm10), eleo lililomwagwa zege linaukubwa wa (1800) chini kuna ujazo wa tabaka la zege ngumu ya jiwe yenye ujazo wa (sm5), baada ya hapo tutaanza kupandishwa nguzo kama ilivyo pangwa.

Tambua kuwa hospitali hiyo inajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m16.166) kimegawanywa sehemu mbili, sehemu ya kwanza jingo kuu ya hospitali lenye ghorofa tatu na tabaka la chini ya ardhi (sardabu), itakua na vitanda vya wagonjwa (230), na sehemu ya pili jengo la utumishi la ghorofa sita litakua na madaktari waliobobea katika fani tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: