Semina ya mbinu za kuandaa mpango kazi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendelea endelevu kinaendesha semina ya mbinu za kuandaa mpango kazi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kuwawezesha kutekeleza wajubu wao vizuri.

Rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema: “Kwa ajili ya kuongeza uwezo wa watumishi katika kuandaa mpango kazi, tunatoa semina ya mbinu za kuandaa mpangokazi kwa watumishi, jambo hilo linaumuhimu mkubwa katika taasisi, kwa kuanzia vipengele muhimu vya mpango kazi kama vime dira na malengo mahsusi, hadi kwenye shughuli za mradi”.

Akaongeza kuwa: “Katika semina hizi tunajitahidi kufundisha kila kitu kipya katika utendaji wa taasisi, ili kuboresha utekelezaji wa majukumu”, akabainisha kuwa: “Hii ni miongoni mwa semina ambazo hufanywa kila mwaka siku tano kwa muda wa saa mbili kila siku”.

Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu huratibu semina na warsha za kujenga uwezo wa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika fani tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: