Chuo kikuu Al-Ameed kimepokea kamati ya wizara yenye jukumu la kupamga idadi ya wanafunzi wanaofaa kupokelewa na chuo kulingana na uwezo wake

Maoni katika picha
Ugeni kutoka kamati ya wizara yenye jukumu la kupanga idadi ya wanafunzi wanaofaa kupokelewa na chuo kulingana na uwezo wake chini ya kanuni za wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, umetembelea chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kufanya ukaguzi wa majengo ya chuo na kukutana na wakufunzi, kukagua uwezo wa chuo katika kupokea wanafunzi wa mwaka wa masomo (2021- 2022m) kwenye kila kitivo, kama sehemu ya kujiandaa na upokeaji wa wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo.

Ugeni huo umepokewa na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na wasaidizi wake, ugeni umekagua maandalizi ya chuo ya kupokea wanafunzi wapya na kuangalia majengo ya vitivo vya chuo kikuu Al-Ameed, aidha umekutana na wakuu wa vitivo na wasaidizi wao pamoja na wakufunzi, kwa ajili ya kubaini idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kupokelewa katika muhula wa kwanza, chini ya vigezo vya wizara.

Mwisho wa ukaguzi wao wamethibitisha kuwa chuo kimeboresha maabara zake na kumbi za madarasa kwa kuweka vifaa vya kisasa, sambamba na kuongeza ukubwa wa madarasa na kumbi zake chini ya mkakati wa upanuzi unaotekelezwa na chuo kikuu Al-Ameed.

Aidha ugeni huo umepongeza mkakati wa elimu uliotengenezwa na chuo, unao endana na mahitaji ya wanafunzi pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi kwenye vitivo vyake.

Uongozi wa chuo umeshukuru ugeni huo na kupongeza kazi kubwa inayo fanywa na wizara, na kwa namna ya pekee ugeni huo kuja kutembelea chuo hiki, katika kuhakikisha ubora wa safari ya elimu hapa chuoni, wamethibitisha kuendelea kuboresha mazingira ya chuo na kuhakikisha kinakua chuo bora hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: