Kufungua semina kuhusu maandishi ya Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefungua semina kuhusu maandishi ya Qur’ani chini ya ushiriki wa wanafunzi wa tawi la Maahadi ya Qur’ani na uangalizi wa walimu waliobobea katika fani hiyo, inalenga kumfanya msomaji kutambua vizuri maandishi ya msahafu na aweze kuyasoma kwa ufasaha.

Nayo ni miongoni mwa semina nyingi zinazo fanywa na Maahadi katika mji mkuu wa Bagdad, semina hii imefanywa katika wilaya ya Husseiniyya kwa mhadhara mmoja kila wiki, idadi kubwa ya wanafunzi wa Maahadi wanashiriki, nayo ni semina ya kwanza ya aina hii hapa wilayani, ambayo watu wanafundishwa kutambua maandishi ya Qur’ani tukufu, sio swala la hati beke yake, bali na vitu vingine.

Wanafundishwa pia alama zilizomo ndani ya Qur’ani na tofauti ya maandishi ya Othmaniy na Imlaaiy, na sifa za maandishi ya Qur’ani pamoja na historia ya kuwekwa alama ndani ya msahafu, sambamba na kuangalia alama zilizopo ndani ya misahafu ya Othmani na maandishi ya Imlaaiy, na kusoma asili ya hati za msahafu na sababu za asili hizo, mosomo yote yanafundishwa kwa kutumia mifano mingi ya Qur’ani tukufu, inayo muwezesha mshiriki kusoma kwa ufasaha.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi katika mji mkuu wa Bagdad hufanya miradi mingi ya Qur’ani katika wilaya ya Karkhi na Raswafa, harakati hizo hufanywa chini ya ratiba maalum inayo lenga kutoa elimu ya msingi katika somo ya Qur’ani tukufu, na kulifanya somo hilo ndio msingi wa kuelekea katika masomo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: