Ugeni kutoka wizara ya kilimo umetembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya viwanda na kilimo

Maoni katika picha
Ugeni kutoka wizara ya kilimo umetembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kilimo na viwanda, kwa lengo la kuangalia maendeleo yaliyo fikiwa na uwezo wa uzalishaji, sambamba na kuangalia teknolojia ya kisasa unayotumika, na mchango wake katika kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa taifa.

Ugeni huo umeongozwa na mwanasheria wa wizara Ustadh Sarmad Muhammad Majidi, sehemu ya kwanza wametembelea vitengo vya shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud, na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Maitham Bahadeli kiongozi mtendaji wa shirika, ameeleza kazi zinazo fanywa na shirika ikiwa ni pamoja na kutengeneza mbolea bora inayo endana na udongo wa Iraq.

Kisha ugeni ukaelekea katika Darul-Kafeel sehemu ya uchapaji na usambazaji wa vitabu, wakaenda pia kutembelea kiwanda cha maji Alkafeel, kote wakapata maelezo kutoka kwa wasimamizi wa viwanda vivyo muhimu.

Mwisho wa ziara yao wameonyesha kufurahishwa na maendeleo waliyo yaona, ambayo yanachangia katika uzalishaji wa taifa na kuongeza uchumi, hasa kwenye sekta ya kilimo na viwanda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: