Kikosi cha washiriki wa semina za Qur’ani kimehitimu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuhitimu masomo ya Qur’ani kwa kikundi cha wasichana, na kuwaingiza katika orodha ya wahitimu na wasomi bora wa Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Wanafunzi (37) kutoka ndani na nje ya Iraq walishiriki katika semina tatu ambazo ni (senima ya Qur’ani tukufu, semina ya usafi, semina ya haki) nazo ni semina maalum kwa kufundisha hukumu za usomaji wa Qur’ani.

Akaongeza kuwa: “Wanafunzi walioshiriki semina tajwa wamefaulu vizuri katika mitihani ya mwisho na kuwa wahitimu bora, semina ya Qur’ani iliandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa kike kutoka Saudia, na semina ya haki ilikua maalum kwa wanafunzi wa kike kutoka Bagdad na semina ya usafi wa Qur’ani ilihusisha wanafunzi wa kike kutoka mkoa wa Najafu”.

Tambua kuwa semina zimeendeshwa na wakina dada waliobobea katika fani hiyo, wakiwa na selebasi maalum ya masomo yote yaliyo fundishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: