Watu wa Karbala na maukibu zao wanajiandaa kuomboleza kifo cha Maasuma (a.s) katika malalo yake takatifu

Maoni katika picha
Watu wa Karbala na maukibu zao kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wamekamilisha maandalizi ya kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Maasuma -a.s- aliyekufa mwezi kumi Rabiul-Awwal 1443h, mbele ya kaburi lake takatifu katika mji wa Qum.

Imeandaliwa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huo yenye vipengele vingi, wakazi wa kitongezi cha Hamza katika mkoa wa Baabil watapokea ugeni wa waombolezaji wa bibi Maasuma na kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) pamoja na watu wa Badra ambao wamechukua jukumu la kuwakaribisha na kuwafanya wahisi huzuni ya msiba huo.

Katika mji wa Qum kutakua na mapokezi kutoka kwa baadhi ya wakazi wa mji pamoja na wairaq wanao ishi hapo, wakiongozwa na muwakilishi wa Atabatu Husseiniyya, kisha yatafanywa maombolezo na kupiga matam chini ya jina la mawakibu za watu wa Karbala.

Baada ya kumaliza kuomboleza ugeni utaenda katika malalo ya Imamu Ridhwa (a.s) kumpa pole kwa kufiwa na dada yake (a.s).

Kitengo kimeandaa usafiri utakaobeba waombolezaji kutoka Karbala hadi kwenye mpaka na Irani, kwenda na kurudi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: