Kuanza semina ya sauti na naghma katika usomaji wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza semina maalum ya (sauti na naghma katika usomaji wa Qur’ani) chini ya ukufunzi wa Shekh Mahadi Qalandar Albayati.

Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi Ustadh Ahmadi Zamili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semina inalenga kuboresha sauti wakati wa usomaji wa Qur’ani kupitia mada tofauti, kama: maqamaat, kusoma kwa maqamaat na lahaja za kiarabu, elimu ya sauti na naghama, au sauti na lahaja, na kuendeleza usomaji na kuboresha viwango vya usomaji wa Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Semina hii itafanywa siku tatu kwa wiki na itadumu kwa muda wa miezi mitano, zitatumika njia za kisasa katika ufundishaji wa sauti na naghma nadhariyya na vitendo, semina hii ni sehemu ya kufanyia kazi maombi ya wasomaji wa Qur’ani, waliotaka kujengewa uwezo katika sekta hiyo, na kutumia njia za kisasa katika kusoma maqamaat na kuzifanyia kazi, miongoni mwa mada kuu zitakazo fundishwa ni: (sifa za sauti za watu, upekee wa sauti na namna ya kuitumia, mazowezi yanayo ongeza pumzi, kufanyia kazi naghma katika Qur’ani).

Pamoja na:

  • - Kutambulisha sauti na kubainisha upekee wake na misingi yake, njia za kukuza sauti na kuilinda.
  • - Kutambulisha naghma za Qur’ani na namna ya kuzifanyia kazi katika usomaji wa Qur’ani tukufu.

Kumbuka kuwa semina zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’ani ni sehemu ya harakati za Qur’ani na semina ni moja ya harakati muhimu, uongozi wa Maahadi unazipa kipaombele zaidi semina za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: