Watumishi wa idara ya usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wamemaliza kusafisha dirisha takatifu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kulinda rangi na muonekano wa madini usiharibike kutokana na kubadilika hali ya hewa.
Kiongozi wa idara bwana Nizaar Ghina Khaliil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hii hufanywa kila baada ya muda na watumishi wa idara yetu, hutumia aina maalum ya visafishio ambavyo haviathiri muonekano wa dirisha, na vinasaidia kuweka muonekano mzuri”.
Akaongeza kuwa: “Kazi ya kusafisha inahusisha sehemu zenye madini katika dirisha, pamoja na paa lake na nguzo, husafishwa kwa umakini mkubwa, na kuondoa kutu na aina zote za uchafu unaosababishwa na mazingira ya hali ya hewa, kwa lengo la kulinda muonekano wake mzuri, na kulifanya liendane na mazingira ya kiroho, kwani huathiriwa na mazindira ya hali ya hewa na sehemu za madini hupata kutu, madini yaliyopo kwenye dirisha hili ni (dhahabu, fedha, silva na madini mengine)”.
Akabainisha kuwa: “Kazi hii hufanywa usiku mwingi kwa ajili ya kuepuka usumbufu kwa mazuwaru, inahatua mbili, hakua ya kwanza kufuta vumbi na pili kusafisha sehemu za dirisha kwa kutumia visafishio maalum”.
Kumbuka kuwa watumishi wa idara wanajukumu la kutoa huduma ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na sehemu iliyotiwa dhahabu (sega la dhahabu) upande wa kibla, huongoza matembezi ya mazuaru eleo hilo wakati wa ziara za kawaida na kubwa zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, huhakikisha watu wanatembea bila kukwama ndani na nje ya haram, hali kadhalika wanajukumu la kudumisha usafi wa dirisha takatifu na uwanja wa haram takatifu na korido zake, bila kusahau kuta, mapambo, milango, taa, viyoyozi na vinginevyo, miongoni mwa vitu vinavyo saidia kuweka muonekano mzuri katika haram takatifu.