(Kanuni za msingi katika kujenga utaratibu wa shughuli za Qur’ani) anuani ya nadwa ya Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya nadwa ya Qur’ani kwa anuani isemayo (Kanuni za msingi katika kujenga utaratibu wa shughuli za Qur’ani).

Mtoa mada alikua ni Dokta Baasim Aabidi, ameeleza njia tofauti za kumuingiza mtu katika uwanja wa Qur’ani na njia za uwasilishaji wa masomo kwa wanafunzi.

Akasisitiza: “Kutumia njia rahisi wakati wa masomo kwa ajili ya kuvuta vijana kuhudhuria semina za kusoma mafundisho ya vizito viwili”.

Kumbuka kuwa nadwa imehudhuriwa na wasomi wa Qur’ani na malezi ya Dini pamoja na kundi kubwa la waumini.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani na kusaidia kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: