Ugeni kutoka chuo kikuu cha Basra: Chuo kikuu Alkafeel kina mazingira mazuri kwa wanafunzi na walimu

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimepokea wageni kutoka chuo kikuu cha Basra ambao ni wakuu wa vitivo na wakufunzi wa chuo hicho, kwa ajili ya kuangalia majengo ya shule na kufungua ukurasa wa ushirikiano.

Ugeni huo umepokelewa na rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani, aliye watembeza sehemu mbalimbali za chuo, kama vyumba vya madarasa, maabara na kwenye mifumo ya kiteknolojia.

Wamefanya makubaliano ya awali ya kubadilishana uzowefu kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu hapa Iraq.

Mjumbe wa ugeni huo Dokta Maazin Auni ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumetembelea chuo kikuu Alkafeel na kuangalia uzowefu wa chuo katika utendaji wake na kubadilishana mawazo na uzowefu, pamoja na kujenga ushirikiano kati ya vyuo vyetu”.

Akaongeza kuwa: “Chuo kinamiliki majengo bora na kinatumia teknolojia za kisasa katika ufundishaji wake, kinamazingira mazuri kwa wanafunzi na walimu, kinafaa kuigwa na vyuo vingene”.

Akamaliza kwa kusema: “Chuo kikuu Alkafeel kinamchango mkubwa katika elimu kupitia sekta binafsi, tunakiombea mafanikio mema, tunatarajia kitaendelea kufanya vizuri katika sekta ya elimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: