Kufanya semina ya kuboresha hati na maandishi

Maoni katika picha
Idara ya turathi za uzuri chini ya ofisi ya habari na maarifa katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, inafanya semina ya kuboresha hati na maandishi, katika semina hiyo wameshiriki baadhi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kuongeza vipaji vyao vya uandikaji.

Semina hii ni sehemu ya harakati za kitengo cha maarifa za kuendeleza vipaji vya uandishi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kuendeleza ushirikiano na vitengo vingine vya Ataba takatifu.

Msimamizi wa semina hiyo muhandisi bwana Muhammad Faalih ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni sehemu ya semina za kitaalamu, inalenga makundi maalum ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya, itaendelea kwa muda wa miezi mitatu, kila wiki kutakua na siku nne za masomo, wanasemina watafundishwa kwa nadhariyya na vitendo kuhusu misingi ya uandishi na njia za kuchora herufi kulingana na maneno, sambamba na mbinu za kuunganisha herufi, na mambo mengine yanayo husu fani hiyo”.

Akasema: “Tumeweka muda wa kuhitimu semina hii kuwa miezi mitatu, muda unaweza kuongezwa kutokana na mahitaji ya wanasemina, tutajitahidi kufundisha kila kitu kwa weledi, tumejiandaa kufanya semina na warsha tofauti zinazo husu fani ya hati za kiarabu na mapambo ya kiislamu”.

Kumbuka kuwa hii sio semina ya kwanza, kitengo cha maarifa kimesha fanya semina nyingi zinazo husu hati za kiarabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: