Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Baabil, imefanya nadwa yenye anuani isemayo: (Fiqhi ya vijana wa chuo).
Nadwa hiyo ni sehemu ya mradi wa Qur’ani vyuoni na kwenye Maahadi za Iraq, mtoa mada alikua ni Dokta Hassan Ma’amuri, ameeleza mambo mengi kwa wanafunzi wa uuguzi, amefafanua mema na maovu.
Nadwa imehudhuriwa na wanafunzi wengi wa kitivo cha uuguzi, mkuu wa chuo Dokta Aminu Yasiri ameshukuru Atabatu Abbasiyya na Maahadi ya Baabil, kwa huduma nzuri wanazo wapa wanafunzi na walimu, akasisitiza umuhimu wa kujenga ushirikiano kati ya chuo na Maahadi.
Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati nyingi zinazo husu Qur’ani pamoja na semina mbalimbali hapa mkoani.
Fahamu kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha kielimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa elimu ya Qur’ani na kuchangia katika kuandaa jamii yenye uwelewa wa mambo yote yanayo husu Qur’ani tukufu.