Kwa maua ya kuzaliwa Zainabu na maneno ya pongezi: yanatolewa katika kupokea mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka idara ya Masayyid, wamesimama kwenye milango yote tangu asubuhi na mapema, wanapokea mazuwaru kwa kuwapa pipi na maua pamoja na kuwaambia maneno mazuri ya pongezi ya kumbukumbu ya kuzaliwa jemedari wa Karbala bibi Zainabu (a.s), aliyezaliwa siku kama ya leo mwezi tano Jamadal-Uula.

Sherehe hii hufanywa kila mwaka, ni miongoni mwa matukio yanayopewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na kufungamana kwake na mwenye malalo hii takatifu Abulfadhil Abbasi (a.s), alikua msaidizi wake na kamanda wa jeshi la kaka yake Imamu Hussein (a.s).

Shughuli hizo ambazo ni sehemu ya harakati za idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, zimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, wametoa shukrani nyingi kwa watendaji, wakasema kuwa pamoja na udogo wake lakini jambo hili lina athari kubwa katika nafsi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: