Wahudumu wa msimamizi wake wanahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa ndani ya haram takatifu

Maoni katika picha
Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya swala ya Isha leo siku ya Ijumaa mwezi (5 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe (10 Desemba 2021m), umeshuhudia hafla ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya, na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu.

Hafla hiyo imehudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru na wahudumu wa malalo tukufu, imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Liith Ubaidi.

Ukafuata ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya, ulio wasilishwa na Shekh Dakhil Nuri kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, akaeleza historia takatifu ya bibi Zainabu (a.s), akafafanua nafasi yake wakati wa baba yake na kaka yake Imamu Hassan (a.s) hadi kufikia harakati ya kaka yake Imamu Hussein (a.s) na kazi kubwa aliyo fanya baada ya kifo cha kaka yake katika ardhi ya Karbala, na jinsi alivyo endeleza na kulinda ujumbe wa kaka yake (a.s) akawa msemaji wa harakati ya Husseiniyya, aidha ameeleza kiwango kikubwa cha elimu aliyokua nayo, ambayo aliichota katika nyumba ya Utume na Uimamu, hakika alikua mhitimu wa shule hiyo, na jinsi alivyokua mfano wa kuigwa katika kujiheshimu, hijabu na Subira.

Baada ya hapo wakapanda kwenye jukwaa washairi wawili, Muhammad Twalibu na Zainul-Aabidina Saidi, wakasoma kaswida zenye mashairi ya kumtukuza bibi Zainabu (a.s).

Hafla ikahitimishwa kwa tenzi zilizo somwa na Ali Abdulhussein na Muhammad Amiri, zilizo onyesha furaha ya waumini kwa tukio hilo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: