Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendelea kufanya mashindano ya (Basi washindane) ya kila mwezi

Maoni katika picha
Idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kufanya mashindano ya kila mwezi ya (Basi washindane) kwa wanafunzi wa tahfiidh.

Mashindano hayo hufanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Alqami chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ushiriki wa wanafunzi wa tahfiidh, kamati ya majaji huuliza maswali tofauti, kama namba za kurasa, aya, mwanzo wa aya na mwisho wake, na mtiririko wa kurasa.

Mashindano hayo yanasaidia kutambua viwango vya wanafunzi na kazi kubwa inayo fanywa na walimu.

Aidha mashindano hayo hulenga kuongeza uwezo wao na kutoa nafasi ya kusoma walicho hifadhi, na kuwashajihisha kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kikanda.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani kupitia matawi yake tofauti, ni kituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kufundisha elimu ya Qur’ani na kuchangia katika kujenga jamii inayo fanyia kazi mafundisho ya Qur’ani, sambamba na uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: