Zaidi ya wanafunzi wa kike 40 wamehitimu semina za hukumu za Qur’ani na tajwidi

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha semina tatu za hukumu za usomaji wa Qur’ani na tajwidi, zilizo pewa majina ya (Twayyibaat, Muhsinaat, Twariqul-Huda), jumla ya wanafunzi (46) wamehitimu katika semina hizo.

Mkuu wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semina hizo zinalenga kujenga utamaduni wa kusoma na kuhifadhi Qur’ani tukufu, na kutambua misingi ya tajwidi na matamshi sahihi ya Qur’ani sambamba na usomaji sahihi kwa ujumla”.

Akaongeza kuwa: “Wakufunzi wa semina hizo ni walimu waliobobea na wenye uzowefu mkubwa, kulikua na mihadhara mingi iliyo endana na umri wa washiriki kama ilivyo pangwa kwenye ratiba, sambamba na mafunzo ya vitengo yaliyo kazia maarifa mafunzo ya nadhariyya, semina zilihitimishwa kwa kutoa mitihani kutokana na masomo waliyosomeshwa kwenye semina”.

Kumbuka kuwa hii ni moja ya semina nyingi zinazo fanywa na tawi la Maahadi, kwa ajili ya kukuza viwango vya usomaji wa Qur’ani kwa kuzingatia hukumu za usomaji na tajwidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: