Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu imeanza kutekeleza mradi wake wa wanafunzi wa vyuo vikuu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imeanza kutekeleza mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi, kwa kufanya nadwa kubwa ya Qur’ani katika kitivo cha famasia kwenye chuo kikuu cha Kufa, iliyohudhuriwa na zaidi ya wanafunzi (300) chini ya uhadhiri wa Sayyid Rashidi Husseini.

Nadwa hiyo imetokana na mkataba wa ushirikiano katika sekta hiyo, baina ya Maahadi na chuo kwa kufanya harakati za Qur’ani ndani ya majengo ya chuo.

Katika mhadhara wake amezungumza kuhusu changamoto za kifikra kwa vijana wa Iraq wa vyuoni, na mashambulizi ya kifikra wanayokumbana nayo, aidha ameeleza njia zinazosaidia kutambua wajibu wa kijana katika kulinda nafsi yake, familia na jamii yake, na kuangalia mambo ya ndani yaliyosambaa katika jamii yetu, akatolea Ushahidi wa aya nyingi za Qur’ani na hadithi za Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Baada ya hapo ukafunguliwa mlango wa majadiliani kati ya mtoa mada na wanafunzi, alipokea maswali yaliyokua ndani na nje ya mada, ambapo alijibu maswali yote na kutoa ufafanuzi zaidi.

Tambua kuwa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi unahusisha harakati mbalimbali, ikiwemo: (kufanya nadwa za Qur’ani ndani ya vitivo na vitengo vyake, mashindano ya kuhifadhi Qur’ani na usomaji, maonyesho ya picha, mashindano ya kuandika Qur’ani, semina za usomaji wa Qur’ani kwa kufuata hukumu za tajwidi na program ya kuendeleza walimu wa vyuo vikuu).

Kumbuka kuwa mradi unalenga kuhuisha harakati za Qur’ani ndani ya vyuo vikuu na Maahadi, kwa madhumuni ya kukuza uwezo wa vijana wetu watukufu, na kuendeleza maarifa ya Qur’ani katika uwanja wa Dini na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: