Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil inafanya nadwa katika chuo cha Qassim

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil inafanya nadwa ya Qur’ani chini ya anuani isemayo: (Utambuzi wa nafsi kwa mtazamo wa Qur’ani na hadithi nuraniyya), ni sehemu ya mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, kwa ushirikiano wa chuo kikuu cha Qassim cha Baabil.

Nadwa imefanywa kwa wanafunzi wa kitivo cha sayansi ya chakula, mtoa mada alikua ni mtafiti Qaisi Masudi, ambaye amebainisha mtazamo wa Qur’ani pamoja na hadithi za Mtume mtukufu, kwa kutaja aya za Qur’ani na haditi tata za Mtume ambazo huwachanganya wanafunzi katika safari yao ya elimu.

Tambua kuwa nadwa hii ni sehemu ya mfululizo wa nadwa za Qur’ani ambazo hufanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake yaliyopo mikoani, kupitia mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, kwa lengo la kufundisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Qur’ani kwa wanafunzi.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha maarifa ya Qur’ani na kuchangia katika kujenga jamii yenye uwelewa wa Qur’ani tukufu na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: