Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inaomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza na kuhudhuriwa na watumishi wa Maahadi pamoja na kundi kubwa la waombolezaji.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Majlisi hii hufanywa kila mwaka, hujikumbusha dhulma alizo fanyiwa Fatuma (a.s) na yaliyo mtokea yeye na familia yake”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na mhadhara kuhusu bibi Zaharaa (a.s), ulioeleza utukufu wake (a.s) na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), sambamba na mambo yaliyotokea baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w) ikahitimishwa kwa utenzi wa majonzi”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa mambo yaliyoshuhudiwa katika majlisi hiyo ni ugawaji wa kadi za pole kwa washiriki, zilizokua zimeandikwa vipande vya khutuba ya bibi Zaharaa (a.s), na mwisho wa majlisi zikasomwa baadhi ya dua na ziara yake (a.s), kisha ikasomwa Duaau-Faraji”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inazingatia kufanya majlisi katika tarehe za matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), huomboleza siku za huzuni zao na husherehekea siku za furaha kulingana na tukio pamoja na muhusika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: