Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutekeleza ratiba yake ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutekeleza ratiba ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) mama wa Abulfadhil Abbasi na ndugu zake walio jitolea Maisha yao kwa ajili ya kuhami ndugu yao Imamu Hussein (a.s).

Ratiba hiyo imeandaliwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya malalo ya mfiwa Abulfadhil Abbasi (a.s), itaendelea kwa muda wa siku tatu, kuanzia leo siku ya Jumamosi (11 Jamadal-Aakhar) hadi (mwezi 13) ambayo ndio kilele cha kumbukumbu ya kifo chake, ratiba hiyo inahusisha utoaji wa mihadhara ya asubuhi chini ya uhadhiri wa Shekh Haadi Zanjiil na mihadhara ya jioni inayo tolewa na Sayyid Nasrat Qashaqsha, kisha hufanywa majlisi ya matam chini ya muimbaji mashuhuri Basim Karbalai.

Kumbuka kuwa mihadhara hii inafanywa chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) unao simamiwa na idara, harakati zake hufanyika mwaka mzima kutokana na matukio ya fivo au kuzaliwa kwa watu wa Ahlulbait (a.s), miongoni mwa matukio muhimu ni hili la kukumbuka kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Kumbuka mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar mwaka wa (64h) mama mtukufu Ummul-Banina mke wa kiongozi wa waumini (a.s) ambaye ni Fatuma bint Hizam Alkilabiyya Al-Aamiriyya, aliyepewa jina la Ummul-Banina kwa sababu alikua na watoto wanne wanaume na wote waliuawa katika vita ya Twafu Karbala, kwa ajili ya kumnusuru bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), mama huyo mtukufu alifia katika mji wa Madina na akazikwa kwenye makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: