Watumishi wa shamba boy la Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweka maua ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na maeneo yanayo zunguka haram hiyo na kwenye barabara zinazo elekea haram, kama ishara ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s), kwa kuzaliwa kwake nuru yake iliangaza mbinguni kama nuru za nyota zinavyo angaza kwa viumbe wa ardhini, hakika nuru yake imeangaza mbinguni na ardhini na viumbe wote wameishuhudia miongoni mwa Malaika, Majini na Binaadamu.
Hakika (a.s) atawaombea msamaha wakosaji miongoni mwa wafuasi wake na kuwatoa motoni kama ndege anavyo chagua mbegu nzuri na kuacha mbaya, wafuasi wake wamekua wakiadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na kuomboleza kifo chake (a.s).
Hivyo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wa kitengo cha utumishi, wamepamba haramu tukufu kwa kuweka maua mazuri, yanayo endana na utukufu wa tukio hili.
Wameweka miti ya mapambo pamoja na maua katika maeneo yote yanayo zunguka Ataba tukufu, na ndani ya hara tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye eneo la katikati ya haram mbili takatifu.