Hivi karibuni katika kituo cha kuhuisha turathi chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimechapishwa kitabu cha (ujembe wa kanuni za kudanganyika) miongoni mwa uandishi wa Sayyid Abdullahi bun Ismaili Bahbahani Annajafiy, aliyekufa mwaka wa 1328h.
Mkuu wa kituo Ustadh Muhammad Wakili amesema “Kanuni za kifiqhi ni msingi mkubwa kwa wanachuoni wa Fiqhi katika kutoa hukumu, kuundwa kwake kunahitaji kazi kubwa na shuhuda nyingi, asilimia kubwa utazikuta kwenye vitabu tofauti vya Fiqhi”.
Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa kanuni hizo ni (kanuni za kudanganyika) zilizo andikwa na Sayyid Abdullahi Bahbahani Annajafiy, alianza na kuzitambulisha, kisha akabainisha mambo yanayo weza kutokea katika kudanganyika, halafu akataja rejea zake, akakamilisha kwa kuandika yanayo husiana na jambo hilo pamoja na masharti yake, akanukuu maoni ya wanachuoni mbalimbali na mijadala yao, na mwisho akaandika maoni yake”.
Kiongozi wa kituo amefafanua kuwa: “Mhakiki wa kitabu hicho Mheshimiwa Shekh Muhammad Issa amekiweka katika nakala tatu, mwanzoni mwa uhakiki wake ameandika historia ya muandishi”.
Kumbuka kuwa machapisho ya kituo cha uhuishaji wa turathi ni sehemu ya matokeo ya mafanikio yaliyo fikiwa na kituo katika sekta ya kuhakiki nakala-kale na vitabu visivyo hakikiwa, na kuviweka katika muonekano mpya na bora zaidi.
