Dondoo za kumbukumbu ya: Mwezi mosi Rajabu kuzaliwa kwa mtu aliyepupia kupata elimu ya watu wa mwanzo na wamwisho

Maoni katika picha
Siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu-Aswabu ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu wa tano Muhammad bun Ali Albaaqir (a.s), aliyezaliwa mwaka wa (57) hijiriyya, watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) walikua wanasubiri kuzaliwa kwake (a.s) kulikobashiriwa na Mtume (s.a.w.w) kwa makumi ya miaka.

Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) ni Imamu wa kwanza mtakasifu aliyezaliwa kutokana na Maimamu wawili watakasifu, ni mtoto wa Ali Zainul-Aabidina mtoto wa Imamu Hussein mjukuu wa Mtume, mtoto wa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), hiyo ndio nasaba yake upande wa baba.

Nasaba yake upande wa mama, mama yake ni bibi mtakatifu Fatuma mtoto wa Imamu Hassan mtoto wa Ali bun Abu Twalib (a.s), alikua ni katika watakatifu wa wanawake wa bani Hashim, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikua anamwita Swidiqah, Imamu Swadiq (a.s) anasema kuhusu mama huyo kuwa: (Alikua Swidiqah hakuna aliyekua kama yeye katika familia ya Hassan -a.s-), yatosha fahari kwake kuwa anatokana na wajukuu wawili wa Mtume (s.a.w.w), na kwamba amelelewa katika nyumba alizo ruhusu Mwenyezi Mungu zijengwe na litajwe jana lake humo, miguu mitakatifu ya mama huyu ndio iliyomlea Imamu Albaaqir (a.s).

Kuniya yake anaitwa (Abu Jafari) hana kuniya zaidi ya hiyo.. amma majina ya sifa (laqabu) anayo mengi, miongoni mwa majina hayo ni: (Al-Amiin, Ashabiihi -kwa sababu alikua anafanana sana na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), Shaakir, Haadi, Swaabir, Shaahid, alipewa jina moja na baba yake la (Albaaqiraini) aidha wanaitwa pia (Albaaqir) na hilo ndio jina mashuhuri zaidi, na jina la (Swadiqaini).

Imamu Albaaqir (a.s) alisoma kwa baba yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s), hadi akawa na elimu kubwa na akawa mashuhuri kuwa anapupia kila elimu, alikua kama alivyo tabiliwa na babu yake Mtume (s.a.w.w) aliye mpa jina la Albaaqir (atapupia katika elimu), alipo bashiri kuzaliwa kwake na kwamba atakuja kuhuisha elimu ya sheria, katika zama ambazo ulimwengu wa kiislamu ulishuhudia mataifa mengi kuingia katika uislamu na kuchanganyika kwa tamaduni na mila mbalimbali.

Imamu Albaaqir (a.s) aliishi na babu yake Imamu Hussein (a.s) miaka mitatu na kidogo, na alishuhudia vita ya Karbala, kisha Akaishi na baba yake Imamu Sajjaad (a.s) miaka thelathini na nane, akasoma kwa baba yake elimu tabia na maadili mema katika jamii, na muda wa Uimamu wake ulikaribia miaka ishirini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: