Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinawapa semina walimu wapya wa shule za Al-Ameed, chini ya mkakati maalum wa kuboresha uwezo wa walimu wao.
Makamo kiongozi wa mafunzo katika kitengo hicho Dokta Hassan Dakhili amesema: “Ratiba hii inasehemu mbili, sehemu ya masomo ya nadhariya na sehemu ya masomo kwa vitendo, masomo yote yameandaliwa kwa mfumo wa majadiliano”.
Akasema kuwa: “Wanufaika wa ratiba hii ni zaidi ya walimu mia mbili wa kiume na wa kike, wakufunzi wa semina hizo ni walimu walio bobea katika sekta ya malezi na elimu, wamesha shiriki kwenye semina nyingi ambazo zimewafanya kuwa na uzowefu mkubwa”.
Akaongeza kuwa: “Tunatarajia semina hizi zinawafaa walimu na kuwakumbusha mambo ya lazima katika kutekeleza majukumu yao ya ulezi na uwalimu kwenye shule za Al-Ameed na kuwafanya kuwa walimu wa kisasa zaidi katika sekta ya ufundishaji”.
Kumbuka kuwa ratiba hii ipo chini ya usimamizi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu, yenye lengo la kuandaa walimu boro wanao endana na maendeleo ya dunia katika sekta ya ulezi na ufundishaji.