Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na kazi ya kuvunja majengo inayomiliki kwa ajili ya upanuzi

Maoni katika picha
Mafundi na wahandiri wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wanaendelea na kazi ya kuvunja nyumba inazo miliki kwa ujili ya kupanua eneo lake.

Upanuzi huo unafanywa upande wa kusini mashariki ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika eneo la baina ya mlango wa Furaat na mlango wa Imamu Ali (a.s) mkabala wake, eneo hilo linamilango mikuu miwili ya kuingia na kutoka mazuwaru na mawakibu Husseiniyya wakati wa ziara kubwa.

Kazi ya kubomoa nyumba hiyo inafanywa kwa umakini na uangalifu mkubwa, kwa kutumia vifaa vya kisasa, kwa sababu nyumba zinazo bomolewa zimeshikana na nyumba zingine, pamoja na kuzingatia kanuni za usalama kwa mazuwaru, ukizingatia kuwa mji huu unashuhudia idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, kutokana na matukio matukufu ya mwezi wa Rajabu-Aswabu.

Kumbuka kuwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kupitia wahandisi na mafundi wake unaendelea kufanya upanuzi wa eneo lake, kwa ajili ya kuingiza idadi kubwa ya mazuwaru hasa wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, sambamba na kutengeneza barabara zinazo elekea kwenye haram tukufu kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyo endana na utukufu wa mji huu pamoja na heshima ya uislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: