Baina ya Imamu Alkadhim na mitume (a.s): Jina la igizo lililofanywa na shule za Dini za Alkafeel za wasichana

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za Dini chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya igizo kwa jina la (Baina ya Imamu Alkadhim na mitume a.s), katika kukumbuka kifo cha mwenye sajda ndefu na mfungwa katika jela yenye giza Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s), aliyeuawa mwezi ishirini na tano Rajabu.

Kiongozi wa idara bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Igizo limefanywa ndani ya ukumbi wa Swidiqah Twahira (a.s) katika mji wa Karbala, waigizaji ni Maukibu ya bibi Maasuma (a.s) chini ya shule ya Ummul-Sibtwain (a.s) katika mji mkuu wa Bagdad, na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wanafunzi na wageni waalikwa”.

Akaongeza kuwa: “Igizo hilo limetumia shuhuda za vitabu vya kihistoria tegemezi, vilivyo andika historia ya Imamu Alkadhim (a.s) na Nyanja anazo fanana na Mitume (a.s), na namna alivyo fanikiwa kufikisha ujembe wake ambao ni muendelezo wa ujumbe wa baba zake na babu zake pamoja na ujumbe wa Mitume (a.s), igizo limeonyesha jinsi alivyo fanikiwa Imamu Alkadhim (a.s) kukwepa vikwazo vya jela, na kufikisha ujumbe wake kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) na dhulma alizo fanyiwa kwa kuwekwa jela, igizo hilo litaonyeshwa dunia nzima ili watu wajue ukubwa wa dhulma walizo fanyiwa Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kuwa walimu kadhaa wameshiriki katika igizo hilo kwenye vipengele mbalimbali, vinavyo onyesha mazingira ya kifo cha Imamu Alkadhim (a.s), sambamba na kutumia mbinu za uigizaji katika kueleza historia ya Maimamu watukufu na changamoto walizopitia katika Maisha yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: