Maelfu wamenufaika na mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alkadhim (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetaja idadi ya wanufaika wa mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alkadhim (a.s), idadi yao imezidi elfu ishirini.

Mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasraawi amesema: “Idadi ya wanufaika ni zaidi ya mazuwaru (20,000), wamefundishwa surat Fat-ha na sura fupi pamoja na nyeradi za swala”. Akasema: “Asilimia kubwa ya wanufaika ni watu wasio jua kusoma wala kuandika, wazee na watu wasiokua waarabu”.

Akaongeza kuwa: “Vituo vya mradi viliwekwa katika barabara zinazo elekea mji wa Kadhimiyya, vilikua vituo (10) na jumla na walimu ishirini”.

Mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani ni sehemu ya mradi wa Tablighi wa hauza ya Najafu.

Mradi unalenga ufundishaji wa Qur’ani na nyeradi muhimu za swala.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani katika sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: