Kamati ya shindano la mazazi matukufu ya Shabaniyya imetangaza majina ya watu wenye majibu sahihi

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia shindano la mazazi matukufu ya Shabaniyya, lililoandaliwa na kitengo cha habari na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya watu wenye majibu sahihi.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati inayosimamia shindano hilo, upigaji wa kura utakao fanya wapatikane washindi kumi na tano, utafanywa jioni ya kesho mwezi (2 Shabani) kwenye hafla kubwa itakayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusherehekea kumbukumbu ya mazazi hayo matukufu, kwenye uwanja wa mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Akaongeza kuwa: Yule ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya wenye majibu sahihi anatakiwa kufika kwenye moja ya vituo viwili akiwa na kitambulisho kinacho onyesha majina yake kamili, ili aingizwe katika orodha ya watakaopigiwa kura, vituo hivyo ni:

Kwanza: Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake, iliyopo katika Atabatu Abbasiyya, mlango wa dhahabu/ mkabala na mlango wa Imamu Aljawaad (a.s).

Pili: Kituo cha mahusiano katika kitengo cha habari, nacho ni maalum kwa wanaume, kipo mlango wa Imamu Ali (a.s), mkabala na Maqaam ya mkono mtukufu wa kushoto.

Mshiriki ambaye hatafika kwenye vituo hivyo jina lake halitaingizwa kwenye orodha ya watakaopiguwa kura.

Kumbuka kuwa zawadi iliyo andaliwa ni (250,000) laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq, na mfuko wa zawadi za kutabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majina ya wenye majibu sahihi yapo kwenye picha ya habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: