Nadwa ya kielimu kuhusu turathi adimu za wanachuoni wa Karbala katika karne ya kumi Hijiriyya

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya asubuhi ya siku ya Ijumaa mwezi (6 Shabani 1443h) sawa na tarehe (11 Machi 2022m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) imefanywa nadwa ya kielimu yenye anuani isemayo: (Utafiti katika turathi adimu za wanachuoni wa Karbala katika karne ya kumi hijiriyya),

Nadwa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha watafiti wakawasilisha fupisho za tafiti zao kama ifuatavyo:

  • - Dokta Rahmani Gharankani/ kutoka chuo kikuu cha Qadisiyya: Ameongea kuhusu utunzi wa mashairi ya kiislamu – amechagua kaswida ya Husseiniyya.
  • - Dokta Abdu-Zahara Zabuun/ kutoka chuo kikuu cha Mustanswiriyya: ameongea kuhusu Ghadiriyya-Kaf’ami na mambo ya kitamaduni.
  • - Dokta Falahu Abdu-Ali Sarkali/ kutoka chuo kikuu cha Karbala:

ameongea kuhusu tafiti za kitabu cha Tasliyatul-Majaalisi na Ziinatul-Majaalisi.

Mlango wa majadiliano ulikua wazi wakati wote wa kikao, wahudhuriaji wamejadiliana na wazungumzaji moja kwa moja, majadiliano yalikua mazuri na yameibua mambo muhimu, wahudhuriaji wamepongeza madhumuni ya nadwa na mada zilizo wasilishwa, wameishukuru sana ofisi ya kituo cha turathi za Karbala kwa kufanya nadwa hii ya kuibua turathi za Karbala, na kuwa chachu ya kupata zaidi hazina za mji wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala kimefanya nadwa nyingi za kitamaduni na warsha za kielimu zilizo jadili turathi za Karbala kwa ujumla, sambamba na kuelekeza macho ya watafiti na wasomi katika kuangalia hazina ya turathi na kuziweka mbele ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: