Kitengo cha habari kimebadilisha muonekano wa mtandao wa kimataifa Alkafeel

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya teknolojia na taaluma ya mitandao katika kitengo cha Habari chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamezindua muonekano mpya wa mtandao wa kimataifa Alkafeel katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s).

Kiongozi wa idara tajwa Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Tumekamilisha usanifu mpya kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika sekta hii, inayo endana na maendeleo ya teknolojia ya mitandao”.

Akaongeza kuwa: “Mpangilio mpya unawezesha huduma nyingi za kihabari, zikiwemo Habari maalum za Ataba tukufu na harakati zake, ikiwa pamoja na maktaba ya picha za mnato, video, matangazo mubashara na mengineyo”.

Akaendelea kusema: “Habari zimeandikwa kwa mfumo mzuri na rahisi, kuna kurasa maalum zinazo eleza huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru, kama vile kitengo cha vitu vilivyo potezwa na mazuwaru, ziara kwa niaba, barua kwa kaburi, maswali na majibu ya kisheria, nyakati za swala na ukumbusho wa matukio ya kidini”.

Tambua kuwa mtandao wa kimataifa Alkafeel, ndio mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu tangu mwaka 2009m, ulipewa jina la (Alkafeel) tangu mwaka (2005m) kabla haujawa mtandao mkubwa wa Habari wenye lugha nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: