Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma kwa mazuwaru wanaokuja Karbala kupitia upande wa Najafu

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tawi la nje uliopo katika barabara ya (Najafu – Karbala), unahudumia mazuwaru wanaokwenda kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwa wanatembea kwa miguu kutoka Najafu.

Huduma zinazo tolewa kwa zaidi ya siku mbili ni chakula, vinywaji, sehemu ya kupumzika, sehemu ya kulala, matibabu na huduma zingine.

Mgahawa ni moja ya kituo muhimu kinachotembelewa na mazuwaru wengi, sambamba na uhusiano wake na jina la Abulfadhil Abbasi (a.s) na uchache wa mawakibu za kutoa huduma katika barabara hiyo.

Watumishi wa mgahawa wamefanya kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru, wanafanya kazi kwa ushirikiano kama nyuki, wanaanza kazi mapema asubuhi hadi usiku wa manane, pale misafara ya mazuwaru inapoisha.

Kumbuka kuwa ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani huwa na watu wengi, na barabara ya (Najafu – Karbala) hutumiwa na mazuwaru wengi, hivyo mgahawa umejiandaa kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru hao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: