Wallahi imevunjika nguzo ya uongofu… wingu la huzuni limetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imevaa vazi la huzuni na majonzi, kuta zake na ukumbi wa malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimewekwa mapambo meusi, kwa ajili ya kuomboleza msiba wa kifo cha wasii wa Mtume (s.a.w.w) mtoto wa Ammi yake, kiongozi wa waumini Ali (a.s), ambaye huanza maombolezo yake mwezi kumi na tisa hadi mwezi ishirini na moja Ramadhani, msiba huu huonekana mpya kila mwaka.

Idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha ushonaji vitambaa na pendera zinazo ashiria huzuni, watumishi wa kitengo cha kusimamia haram wameweka vitambaa na bendera hizo kwenye maeneo ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama ishara ya kuomboleza msiba huu na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu, yenye vipengele vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: