Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutekeleza ratiba ya semina ya (Juu ya mwenendo wako ewe kiongozi wangu) kwa baadhi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya wakike, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwafundisha namna ya kupambana na changamoto za Maisha katika mambo binafsi, kijamii, malezi ya watoto na kila kinacho fungamana na familia.
Kiongozi wa kituo hicho bibi Sara Haffaar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni moja ya semina za kitaalam zinazofanywa na kituo, kwa kundi la wanawake wenye umri tofauti, semina hii ni maalum kwa ajili ya wanawake wanaotoa huduma Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kuwajengea uwezo katika kupambana na changamoto binafsi, za familia na jamii”.
Akaongeza kuwa “Semina inafanywa ndani ya ukumbi mkuu siku mbili kwa wiki na itadumu kwa miezi miwili mfululizo, semina inamfululizo wa mihadhara isemayo (Nani wewe?) inayotolewa na Dokta Shimaa Nasoro bingwa wa maswala ya saikolojia, anaongea kuhusu umuhimu wa kujitambua, na masharti muhimu kwa kila mtu anaetaka kufikia malengo yake katika Maisha”.
Kumbuka kuwa semina hii ni sehemu ya harakati za kituo zinazolenga kufundisha utamaduni bora wa Maisha ya kifamilia kwa wanawake na jamii, kwa ajili ya kuweka maelewano katika familia na jamii, semina zote huendeshwa chini ya wasomi waliobobea na wenye uzowefu mkubwa unaowawezesha kutekeleza jukumu lao kwa ufanisi.