Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inafanya warsha za kuwajengea uwezo walimu wa Qur’ani katika mikoa miwili Misaan na waasit.
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema: “Tunafanya warsha hizi kwa ajili ya kuboresha walimu, ili waweze kuwapa elimu bora wanafunzi wetu watukufu”. Akaongeza kuwa: “Tunatarajia kuhitimisha kundi kubwa la vijana kila mwaka wanao ingia katika jamii wakiwa na elimu nzuri ya Qur’ani”.
Akaendelea kusema: “Warsha zinafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Qur’ani tukufu ni msingi wa Imani na ngao ya jamii)”.
Washiriki wamepongeza ratiba hii na kusema inamchango mkubwa katika uislamu na kwenye sekta ya Qur’ani tukufu.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani ni sehemu ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya yenye jukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii yenye ya wasomi wa Qur’ani katika kila sekta.