Makumbusho ya Alkafeel inafanya nadwa ya kielimu ya tano

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumamosi imefanya nadwa ya tano kwa jina la (Mambo ya msingi kwa makumbusho yenye mafanikio).

Rais wa makumbusho hiyo Swadiqu Laazim amesema: “Nadwa hii ni sehemu ya maazimio yaliyowekwa kwenye kongamano la makumbusho la kimataifa, lengo la nadwa hii ni kufundisha utamaduni wa makumbusho na turathi kwa wadau wa makumbusho”.

Akaongeza kuwa: “Nadwa ya leo imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya uhadhiri wa Dokta Mundhiru Mundhiri makamo wa kiongozi mkuu wa kitivo cha Adabu/ katika chuo kikuu cha Bagdad, nadwa imefanywa kwa njia ya mahudhurio ya moja kwa moja na njia ya mtandao wa (zoom)”.

Akaendelea kusema: “Tunakipengele cha kutembelea makumbusho, jambo hilo linaimarisha utaifa kwa kutambua turathi za Iraq”.

Kumbuka kuwa tumeshaweka ratiba maalum ya kufanya nadwa hizi zitakazo kuwa na maudhui tofauti, kila mwezi tutafanya nadwa mara moja au zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: