Mradi wa kiongozi wa wasomaji umekamilisha maandalizi ya kuanza kwa awamu ya sita

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kuanza kwa hatua ya sita ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa taifa.

Kikao cha mwisho kimehudhuriwa na rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali na watumishi wa kituo wakiwemo walimu na wasomaji.

Mkuu wa kituo Sayyid Hasanaini Halo ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya mradi huo, sambamba na kukamilika mialiko ya baadhi ya wasomi wa Qur’ani watakao shiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Mwisho wa kikao hicho rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Mustaqu Ali akasema yuko tayali kutoa msaada wowote utakaohitajika, ili kuboresha awamu hii na kuhakikisha washiriki wake wanakuwa vinara wa usomaji wa Qur’ani katika taifa hili.

Kumbuka kuwa mradi huu unasimamiwa na walimu mahiri, unalenga kutengeneza kizazi cha wasomi wa Qur’ani, kwa kuandaa vijana wadogo wenye vipaji vya usomaji wa Qur’ani na kuwapa semina fupi za kuendeleza vipaji vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: