Makatibu wawili wakuu wa Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya wamepeana pongezi za Iddi mbele ya viongozi wa kamati zao za utawala na marais wa vitengo.
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini ndani ya ukumbi wa utawala, asubuhi wa Jumapili amepokea pongezi kutoka kwa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Ustadh Hassan Rashidi Al-Abaiji na wajumbe fuatana nao.
Baada ya Adhuhuri ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ukiongozwa na katibu mkuu wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo ukaelekea Atabatu Husseiniyya kutoa pongezi kwa kuingia sikukuu tukufu ya Iddul-Adh-ha.
Wakapokewa na makamo katibu mkuu Dokta Alaa Ahmadi Dhiyaau-Dini na baadhi ya viongozi, mapokezi hayo yalifanywa baada ya kumaliza kufanya ziara na kusoma dua mbele ya malalo ya Imamu Hussein (a.s).
Kikao chao kimeshuhudia maneno mazuri ya kupongezana kutokana na sikukuu ya Iddul-Adh-ha tukufu, na kujadili njia za kuimarisha ushirikiano baina ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na kila kinachoweza kusaidia kutoa huduma bora kwa mazuwaru.