Idara ya Tablighi chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na semina elekezi kwa watumishi wa Ataba, hii ni semina ya kumi na nne.
Kiongozi wa idara Sayyid Muhammad Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni semina muhimu inayofanywa katika eneo takatifu, kwa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tunawajengea uwezo wa maarifa ya dini na utamaduni”.
Akaongeza kuwa: “Muda wa kila semina ni siku kumi na tano, huwa na ratiba maalum yenye masomo tofauti ya Fiqhi, Aqida, Utamaduni, Akhlaqi, Midahalo na kipindi cha maswali na majibu”.
Akaendelea kusema: “Semina hizi zinalenga kuwa na watumishi bora katika jamii, ukizingatia kuwa wanafanya kazi katika eneo takatifu, mambo ya Dini, Fiqhi, Aqida kila mtu anayahitaji na watumishi wanatakiwa kujinoa katika mambo hayo kila wakati”.
Kumbuka kuwa semina hizi ni sehemu ya harakati ya idara ya Tablighi, zimeanza kutolewa muda mferu, na bado zinaendelea kutolewa kwa watumishi wa Ataba tukufu na kuwafanya waendane na utukufu wa eneo loa la kazi.