Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanya upasuaji wenye mafanikio kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka minne aliyekua na tatizo la kukauka kwa ute kwenye mfupa wa mgongoni kwa kumuwekea ute wa kutengenezwa.
Madaktari wamesema kuwa mgonjwa alikua anapata maumivu makali sana chini ya mgongo, hadi alikua hawezi kutembea na kufanya kitu chochote.
Baada ya kufanyiwa vipimo daktari bingwa wa mifupa Dokta Khalidi Siraji amesema, “Tulimuandaa mgonjwa kwa ajili ya upasuaji, tukamfanyia upasuaji na kuweka ute wa kutengenezwa sehemu zilizokua zimekauka”.
Akasisitiza kuwa: “Upasuaji umefanikiwa na mgonjwa ametoka akiwa na afya nzuri”, akasema “Vifaa-tiba vya kisasa tulivyo navyo vinamsaada mkubwa wa kufanikisha upasuaji wa aina mbalimbali unaofanywa hapa hospitali”.