Maandalizi ya ziara ya Arubaini.. kitengo cha majengo ya kihandisi kimekamilisha ujenzi wa daraja la chuma

Maoni katika picha
Kitengo cha majengo ya kihandisi kimekamilisha ujenzi wa daraja la chuma litakalo tumika kwa muda na mazuwaru, kama sehemu ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Daraja lipo upande wa madharibi ya Atabatu Abbasiyya tukufu mkabala na mlango wa Imamu Hassan (a.s), hujengwa kila mwaka na mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Ataba tukufu, kabla ya kuanza msongamano wa mazurwaru wanaowasiri Karbala.

Daraja hilo linasaidia kuondoa msongamano wa mazuwaru na kuepusha muingiliano baina yao na matembezi ya mawakibu za kuomboleza zinazo ingia kwenye uwanja wa haram tukufu kupitia upande wa kusini magharibi, upande wa mlango wa Imamu Hassan na Imamu Hussein (a.s).

Daraja hilo hufungwa kwa vipande vya vyuma, huunganishwa kwa ustadi mkubwa wa kihandisi, linaupana wa mita (8) na urefu wa kwenda juu zaidi ya mita (4), pande zake mbili huwekwa mbao zinye ukubwa wa (mt 1.22 x mt 2.40).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: