Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume mtukufu

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), majlisi hii hufanywa kila mwaka katika siku ya kumbukumbu ya kifo cha mbora wa Manabii na Mitume.

Kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya Shekhe Abduswahibu Twaiy amesema: “Idara yetu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu kwa kufanya majlisi ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa “Mjlisi hiyo ni katika mradi ya Ummul-Banina (a.s) unaohusu uhuishaji wa matukio ya Ahlulbait (a.s), likiwemo tukio hili, majlisi itafanyika kwa siku tatu, kila siku itakua na mihadhara miwili”.

Akabainisha kuwa “Mhadhara wa kwanza unatolewa baada ya swala ya Dhuhurain na Shekhe Mustafa Fartusi na mhadhara wa pili unatolewa baada ya swala ya Isha na Shekhe Ali Khafaji ukifuatiwa na kaswida kutoka kwa Muhammad Tarhini”.

Kumbuka kuwa kifo cha Mtume Muhammad bun Abdullahi (s.a.w.w) kilitokea (mwezi ishirini na nane Safar mwaka wa 11 h) akiwa na miaka (63), wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kumbukumbu hii huenda kwenye kaburi la Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) katika mji wa Najafu, kumpa pole kwa kufiwa na kaka yake Mtume Muhammad (a.s), nayo ni miongoni mwa ziara maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: