Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askari.. Atabatu Abbasiyya imetoa kikosi cha kusaidia kutoa huduma

Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma kikosi cha watumishi wake kutoka vitengo tofauti kwenda kusaidia watumishi wa Atabatu Askariyya kutoa huduma mbalimbali wakati huu wa kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askari (a.s) katika mji wa Samaraa.

Rais wa ujumbe huo Sayyid Ahmadi Shaakir Hashim amesema “Ugeni huo unahusisha watumishi wa kitengo cha kulinda nidham, watumishi wanaosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kitengo cha kusimamia haram, kitengo cha utumishi, kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, kitengo cha mitambo na mawakibu za kidini na idara ya madaktari, vitengo vyote hivyo vinashiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa maimamu wawili watakatifu”.

Akaongeza kuwa “Sehemu ya huduma wanazotoa ni kutembea pamoja na mazuwaru kwa lengo la kulinda amani baina yao, yaani wanafanya kazi kama askari kanzu, kwa lengo la kuangalia mambo yasiyofaa kwa mazuwaru na kuripoti katika Atabatu Abbasiyya ili hatua za haraka zichukuliwe kuzuwia tatizo linaloweza kutokea”.

Akaendelea kusema “Tumeongeza nguvu kwenye idara ya usafi na kugawa maji, tumetoa gari nne za kubeba taka na gari sita za kusambaza maji, pamoja na gari zingine kwa ajili ya kubeba mazuwaru bure, kutoka sehemu zinapo ishia basi hadi karibu na maimamu wawili (a.s)”.

Akabainisha kuwa: “Kikosi cha madaktari kimeandaa vifaa vinavyo hitajika kutolea huduma za afya wakati wowote ambapo zaairu anaweza kupata tatizo la afya wakati wa matembezi ya kuingia kwenye Atabatu Askariyya au kutoka”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: