Baada ya ufunguzi wa dirisha jipya la malalo yake takatifu.. Atabatu Abbasiyya imeupongeza uongozi wa Atabatu Zainabiyya tukufu

Baada ya kumaliza shughuli za ufunguzi wa dirisha jipya la malalo ya Aqilah Zainabu (a.s) Atabatu Abbasiyya imeupongeza uongozi wa Atabatu Zainabiyya tukufu.

Sayyid Kadhim Abadah mjumbe wa idara ya uongozi na msimamizi wa utengenezaji na ufungaji wa dirisha jipya la malalo ya Aqilah Zainabu (a.s) amesema: “Idara ya Abbasiyya baada ya kumaliza kazi ya ufungaji wa dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s) inatoa pongezi nyingi kwa idara ya Atabatu Zainabiyya kwa kazi kubwa waliyofanya katika ufungaji wa dirisha jipya”.

Akaongeza kuwa “Hakika ushirikiano mkubwa uliokuwepo kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu Abbasiyya na Zainabiyya ndio sababu kubwa iliyopelekea kumaliza kazi ya ufungaji wa dirisha ndani ya muda mfupi, hakika ushirikiano huo umekuwepo toka mwanzo wa utengenezaji wa dirisha hilo tukufu hadi mwisho kwenye kazi ya ufungaji wa dirisha”.

Siku ya Jumapili ilifanywa hafla ya ufunguzi wa dirisha hilo ndani ya malalo ya bibi Zainabu (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umesisitiza kuwa “Hakika maeneo yetu matakatifu hayawezi kutenganishwa na utambulisho wa uislamu na ubinaadamu, ni anuani ya Imani yetu na uwepo wetu, miongoni mwa maeneo matakatifu ni makaburi ya Ahlulbait (a.s), ambao Mwenyezi Mungu amezifanya nyoyo za wafuasi wao kumiminika kwao, na kuwa sehemu ya uwepo wa ubinaadamu na anuani ya Dini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: