(Mchinjwa wa Furaat) Filamu fupi iliyotengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu

Kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimekamilisha utengenezaji wa filamu fupi iitwayo (Mchinjwa wa Furaat).

Mtengenezaji wa filamu hiyo Sayyid Azharu Khamisi amesema “Filamu imetumia visa vya kweli vilivyotokea kwenye ziara za Arubani zilizofanywa karne iliyopita, riwaya za waingereza zilikua zinasema kuwa mbingu ilinyesha damu mwaka 685 miladiyya sawa na mwaka 61 hijiriyya, ambao ndio mwaka aliouawa kishahidi Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kituo cha uzalishaji Alkafeel chini ya kitengo cha Habari kimetengeneza filamu fupi ya tukio hilo, kipo hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa filamu hiyo”.

Akabainisha kuwa “Filamu imerekodi maeneo ya kihistoria katika mji mtukufu wa Karbala, ameteuliwa muwakilishi As’adi Abdulmajidi kuwa kamanda wake na Sayyid Muhammad Shimri mkuu wa idara ya picha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: